Traduit en Kiswahili
Par L'Observatoire des Langues (Ministère de la Culture et des Arts)

Wanawake Amani na Kimya

Kusudio la Baraza la Usalama, 1325
(2000)

Baraza la Usalama

Limakumbusha makusudio 1261 (1999) ya tarehe 25 agosti 1999, 1265 (1999) ya tarehe 17 septembri 1999, 1296 (2000) ya tarehe 19 aprili 2000 na 1314 (2000) ya tahere 11 ogosti 2000, pia matangazo ya Mwenyekiti kuhusu jambo hili; linakumbusha tena tangazo la Mwenyekiti mbele ya magazeti siku ya Silu kuu ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za wanawake na amani kati ya mataifa (Siku kuu ya mwanamke ya kimataifa); tarehe 8 marsi 2000 (SC/6816),

Linakumbusha tena ahadi za Tangazo na za Mpango wa kazi wa Beinjing (A/52/231) pamoja na zile zilimo katika matini iliyokubaliwa na Mkusanyiko wa kawaida katika mkusanyo maalumu wa 23 unaoitwa "Wanawake katika mwaka wa 2000: usawa wa jinsia, maendeleo na amani kwa karne ya XXI" (A/S-23/10/Rev.1), hasa ahadi zenye kuhusu wanawake na vita,

Linafahamu shabaha na kanuni zilizotelewa katika Katiba ya Umoja wa Mataifa na linawaza kama Katiba inalipa Baraza la Usalama wajibu mkubwa ya kulinda amani na kimya kati ya mataifa,

Linashurulika kwa kuona kama idadi kubwa vibaya vya vita, iwe wakimbizi kama vile wake waliohamishwa, ni raia, hasa wanawake na watoto, na kama wapigani na wale wenye silaha wanazoea zaidi na zaidi kuwageuza shabaha zao, na linafahamu vinyume vyenye kutokea na hayo katika kazi za kuleta amani ya kudumu na kuwapatanisha watu,

Linahakikisha ukubwa wa kazi ambayo wanawake wana katika kuzuia na kutengeneza matatizo ya vita, na katika kuimarisha amani, na linasisitiza kama ni lazima wanawake washiriki kwa usawa katika juhudi zote za kutafuta kulinda na kuendelesha amani na kimya, na washiriki kweli, na kama inafaa washiriki zaidi katika mashuruli ya kukata shauri ili kuzuia na kutengeneza mambo ya magomvi,

Linahakikisha pia kama ni lazima kuheshimu bila msito mipango ya Sheria ya kimataifa kuhusu binadamu na kanuni zenye kuhusu hali za binadamu na kukinga hali za wanawake na za watoto wanawake wakati wa vita na kisha vita,

Linasisitiza ya kwamba wale wote wenye kuhusika wanapashwa kushurulika kwa ginsi mpango wa kufukwa silaha za kuzikwa na wa kufundisha watu hatari ya silaha hizo iangalie pia hasa mahitaji ya wanawake na ya watoto wanawake wadodo,

Linawaza kama inafaa, kwa haraka, kushurulikia kuingiza wanawake katika kazi za kulinda amani, na kwa hiyo, linakubali Tangazo la Windhoeck na Mpango wa kazi wa Nanibia kuhusu shuruli la kutia usawa kati ya jinsia katika kazi mbalimbali za kuleta amani (S/2000/693),

Linaona lazima ya ombi ambalo lilifanyiwa na Mwenyekiti mbele ya watungamagazeti tarehe 8 marsi 2000, la kusema kama wote wenye kuhusika na kazi za kulinda amani wapate mafundisho maalumu kuhusu kukinga, mahitaji maalumu na haki za msinji za wanawake na watoto katika hali ya vita,

Linawaza kama kazi ya kulinda na kuendelesha amani na kimya kati ya mataifa ingekuwa rahisi, kama watu wengeelewa zaidi vinyume vya vita kwa wanawake na watoto wanawake wadogo, kama kungekuwa mapatano yenye kufuata kanuni na yenye mafaa ili kuahidi kuwakinga, na kama wanawake wangeshiriki kweli katika kazi ya kuleta na kulinda amani,

Linaona kama ni lazima kuwa na maelezo kuhusu vinyume vya vita kwa wanawake na watoto wanawake wadago,

Ndiyo sababu :

Ni lazima kua viombo kuhusu kinyume kia vita juu wanawake na watoto wanawake.

1. Inaomba bila shaka kwa Nchi-wanamemba wanawake wawe wenyi katika daraja mbali mbali za huduma za kila nchi, wilaya na za kimataifa kwa ajili ya kuarifu, kumiliki na kutafuta kumaliza migogoro.

2. Inamwamria Katibu Mkuu afwatilie mipango yake (A/49/587) inayotangulisha wanawake washiriki zaidi katika Komiti kunakokamatika mipango ya kumaliza vita na wachungulizi wa amani.

3. Inaomba bila shaka kwa Katibu Mkuu awatie zaidi wanawake katika wasimamizi na watumwa wa kipekee kwa ajili ya majadiliano. Vile inaombwa kwa Nchi-Wanamembe zijulishe kwa katibu Mkuu majina ya wanawake wanaoweza kupatikana kwa orodha, yake inayoweza kubadilishwa mara kwa mara.

4. Inaomba bila shaka tena kwa Katibu Mkuu atafute namna yakuongeza kazi na ufundi wa wanawake katika vitendo vya Umoja wa mataifa hasa kama vile wachunguzi wa kiaskari, wanamemba wa kipolisi, wataalamu wa haki za binadamu na wachunguzi wa hali za kibinadamu.

5. Inajitangaza tayari kwa kuingiza katika Umoja wa Mataifa, mwenendo unaohuzunika na usawa kati ya wake na wanaume katika uchunguzi wa anami. Inaomba pia kwa katibu Mkuu, ikiwezekama, awe mwangalifu ili katika vitendo vya Umoja wa Mataifa kupatikane vikundi vya wanawake.

6. Inaomba kwa Katibu Mkuu ajulishe kwa Nchi-Wanamemba mipango na mafundisho yanayoelekea haki na lazima za pekee za wanawake, pia mafaa ya wanawake ya kupatikana katika vikundi vya kuungua na kusimamisha amani. Inaalika Nchi-Wanamemba kuingiza vitendo vile na pia vitendo vya kwarifu ugonjwa wa ukimwi VIH/SIDA katika ratiba za nchi. Ratiba hiyo ya elekea pia wanajeshi na wanapolisi wanaojitayarisha kwa kutumwa. Inaalika tena kwa Katibu Mkuu awe muangalifu ili mafundisho hayo itolewe kwa namna moja kwa walinzi kiraia wa amani.

7. Inaomba bila shaka kwa Nchi-wanamemba ziongeze misaada yao ya pesa, ya ufundi na ya vyombo kwa ajili ya kusaidia vitendo vya kufundisha usawa kati ya wake na waume na vitendo vinavyofwatana na vile vya UNICEF (huduma ya Umoja wa Mataifa inayohusika na watoto wadogo), vya HCR (huduma ya Umoja wa Mataifa inayokusika na wakimbizi) na vingine.

8. Wakati kunafanyika majadiliano na kutimizi makubaliano ya amani, Inaomba kwa wote waweze kuchagua mwenendo unaoshurulika na usawa kati ya wake na waume, zaidi :

a)kuzingatia lazima za kipekee za wanawake na za wasichana wadago wakati wanaparusishua na kuwekwa nchini mwao, kwa ajili ya kukomboana, kuikalishwa na kujenga tena baada ya migogoro,

b)kuchagua makusudi yanayotegemea maangilio ya amani yaliyoshikwa na vikundi vya wanawake na mienendo ya kumaliza magombezi pia. Kufanya kwa ginsi wanawake wapatikane katika mitambo ya kutimiza makubaliano ya amani.

c)kuchagua makusudi zinazotadariki ukingo na heshima ya haki za msingi za wanawake na za wasichana wadogo, zaidi katika mambo ya katiba, uchaguzi, ya kipolisi na ya sheria.

9. Inaomba kwa vikundi vyote katika migogoro ya vita viheshimu kwa kamili sheria ya kimataifa inayoelekea haki na ukingo wa wanawake na wasicharia wadago, hasa kabisa raia, kwa mfano mapashwa yanayowaelekea kufwatana na Masikilizano ya Genèva ya 1949 na Yale yaliyoongezwa ya 1977, na Masikilizano ya 1951 ambayo yanaelekea hali ya wakimbizi na ya Masikilizano yaliyoongezwa ya 1991, pia na Masikilizano ya Umoja wa Mataifa ambao inaelekea hali za mtoto ya 1989 na Yale yaliyoongezwa (mawili), lakini yasio mhimu ya tarehe 25/05/2000, na Inaomba pia kizingatia mipango mhimu ya Mapatano ya Roma kwenye Baraza la hukumu la kimataifa.

10. Inaomba kwa vipande vyote vinavyopatikana katika migogoro vita kukamata hasa mipango inayowakinga wanawake na wasichana wadogo kwa vitendo vya kuingiliwa kwa kinguvu na wanawume, hasa mapenzi ya kinguvu na vitendo vingine vya namna moja wakati wa vita;

11. Inatia mkaazo kwa Nchi zote zinazo mapashwa ya kumaliza ukosefu wa azabu na kuwaamua waliotenda vitendo viovu vinavyofwatana na mauaji kwa kikabila, kwa vita, na hali yote ya mapenzi ya kinguvu na wanawake na wasichana wadogo. Basi kwa vile, watenda vitendo hivyo wasihurumiwe,

12. Inaomba kwa vipande vyote katika vita viheshimu hali ya kiraia katika kambi waliyomo wakimbizi wa vita na kuzingatia lazima za kipekee za wanawake na wasichana wadogo wakati watapojenga makambi hayo, kwa kufwatana na mipango namba 1208 (2000) ya tarehe 12/04/2002;

13. Inalazimisha wale wote walio na mipango ya kunyanganya silaha wasisahau lazima mbalimbali za wanawake na wanaume waliokuwa waaskari na pia wale wanaokaa nao wakati watapotoka jeshini na kurudi katika maisha ya kiraia,

14. Inajitangaza tena kuwa tayari kwa kujifunza kinyume ya mipango yote juu ya jamii, kwa kufwatana na kifungo 41 cha Umoja wa Mataifa kadiri ya lazima ya kipekee za wanawake na wasichama wadogo;

15. Iko tayari kwa kuchungulia usawa kati ya wake na wanume, hasa haki za wanawake kwa kufwatana na majadiliano ya vikundi vya wanawake nchini na mataifa mengeni;

16. Inaalika Katibu Mkuu ajifunze vinyume vya migogoro ya vita juu ya wanawake na wasichana wadogo, kazi ya wanawake katika ulinzi wa amani na kati ya mienendo ya amani na ya kumaliza magombezi. Inamualika pia Katibu Mkuu aitolee ripoti mwisho wa kazi hiyo ili aitangaze kwa nchi zote wanamemba wa umoja wa Mataifa,

17. Inaomba kwa Katibu Mkuu, ikiwezekana, awake katika ripoti yake maelezo yanayoelekea usawa kati ya kiume na kike katika uchungulizi wote wa kulinda amani na vipengele vyote vinavyoangalia wanawake na wasichana watoto;

18. Inakamata mpango wa kubaki kilamara msikilivu wa swalihilo.

Kwa kupata maelezo zaidi, uchungulie www.un.org/womenwatch .

Imejulishua na Chumba cha ujulishi cha Umoja wa Mataifa
DPI/2238-octoba 2001-10M.

Kwa mara ya kwanza, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilichungua swali kuhusu " wanawake, amani na kimya ", hapo mji New York, tarehe 24 na 25 oktobri 2000.
Ilikuwa ni jambo la kuonyesha maendeleo katika historia. Mazungunzo yalihusu mahitaji ya wanawake katika kazi zote za Umoja wa Mataifa za kulinda amani, na pia jambo la kawaida ambalo ni lile la kazi ya wanawake katika shuruli la kuimarisha na kulinda amani. Wengi katika hotuba zao walisisitiza kama inafaa kuwashirikisha wanawake katika mitindo yote ya kazi za kuimarisha amani, na waliomba hasa washiriki katika kazi za kukata shauri.

Tarehe 31 oktobri 2000, Baraza la usalama lilikubali, kwa umoja, kusudio 1325 (2000) kuhusu wanawake, amani na kimya Kusudio hilo liliomba kwa watu wote ambao wanapashwa kushurulikia katika majadiliano na kufuata mapatano juu ya amani wafuate njia yenye kushurikia usawa kati ya jinsia na mahitaji maalumu ya wanawake na wasichana wakati wa kuwarudisha kwao na wa kuwapa makao, wa kuwatosha katika hali fulani, wa kuwarudisha katika jamii yao na kutengeweza inchi kiisha mapingano. Kukubaliwa kwa kusudio hili lenye maana katika historia kulikuwa hatua muhimu katika historia kulikuwa hatua muhimu katika njia ya kutambua ukubwa wa kazi ya wanawake katika kazi ya kutengeneza maneno ya magomvi, ya kulinda amani na kuimarisha amani kisha vita.

Hapa chini mnaweza kusoma matini ya kusodio hilo la Baraja la Usalama.